Msanii wa Bongo Flava maarufu kwa nyimbo yake ya “You” Bruce Africa, ame tangaza ujio wa EP yake mpya itakayo julikana kwa jina la “Boyfriends Life EP”.
EP hiyo ambayo inakuja na nyimbo mpya 6, inatarajiwa kutoka siku ya ijumaa ya tarehe 27 mwezi huu wa tisa, huku ikiwa na sauti kutoka kwa wanamuziki wengine kutoka East Africa ambao ni G Nako kutoka Tanzania, Vijana Barubaru kutoka Kenya, na John Blaq kutoka nchini Uganda.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bruce ameandika “Hello World, Experience the undeniable growth and the work of art from me through this marvelous Ep,Boyfriends Life Ep. Stay tuned (27.09.24)” akamaliza kwa kuwataja watayarishaji walio husika kutengeneza EP hiyo ambao ni @dracobeatz1 @wambaga_tz na @blvcq_igbo6.
Endelea kutembelea Audio Mpya, ili kuwa wa kwanza kusikiliza EP hii mpya pale itakapo toka rasmi siku ya tarehe 27 mwezi huu.